Jumatatu , 8th Apr , 2024

Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe linamshikilia, Edger Mkane (23) mkazi wa Mtaa wa Kisiwani Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani humo kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa darasa la saba (11) kwa kuahidi kumpa shilingi 1,500.

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Njombe, Kamishna Msaidizi Mahamoud Banga amethibitisha kuwa tukio hilo limetokea Aprili, 04 mwaka huu 2024 majira ya saa nane mchana.

Amesema mtuhumiwa na mwanafunzi anayedaiwa kubakwa ni mtu na binamu yake, hivyo mwanafunzi huyo alikwenda kuangalia televisheni nyumbani kwao na mtuhumiwa ndipo tukio hilo likatendeka.

Aidha, amebainisha kuwa tukio hilo bado halijathibitika kidaktari, hivyo kuleta ukinzani kati ya taarifa inayotolewa na daktari na ile inayotolewa na wahusika.