Jumamosi , 13th Nov , 2021

Njia ya wapita kwa miguu ya mtaa wa Nyamrugo, manispaa ya Bukoba iliyokuwa imefungwa na mchungaji wa kanisa la Chemchemi Israel Mlaki, imefunguliwa baada ya viongozi wa manispaa hiyo kufika na kuviondoa vizuizi vilivyokuwa vimewekwa na mchungaji kwa madai ya kwamba hilo ni eneo la kanisa.

Mchungaji wa kanisa la Chemchemi Israel Mlaki

Wakizungumza baada ya vizuizi hivyo kuondolewa, baadhi ya wananchi wa mtaa huo wamesema kuwa wameteseka kwa muda mrefu na sasa wanaona kama wamepata Uhuru, huku mchungaji Mlaki anayedaiwa kuziba barabara hiyo akikataa kuhojiwa.