Jumatatu , 26th Sep , 2022

Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam limemkamata Tazarn Alfan Mwambengo (27), mkazi wa Ukonga, ambae anatuhumiwa kusambaza taarifa za uongo kuhusu kifo cha Dkt. Harrison Mwakyembe kupitia chaneli ya televisheni ya mtandaoni jambo ambalo si la kweli.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Jumanne Muliro

Katika chanel hiyo ya mtandao mtuhumiwa huyo aliandika “BREAKING NEWS HUZUNI YATANDA MAZISHI YA MWAKYEMBE” taarifa ambazo ziliibua  taharuki kubwa kwa wananchi hasa kwa Dkt Mwakyembe mwenyewe na familia yake.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es Salaam linamshikilia  Innocent Adam Chengula, Mhehe, 23, mkazi wa Kigogo  Luanga, amekamatwa kwa tuhuma za kujinasabisha kuwa yeye ni Dkt. HASSAN  ABBAS Katibu Mkuu Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kupitia mtandao na kutumia laini za simu zenye usajili usio na majina yake.

Mtuhumiwa huyu amekuwa akiweka picha na majina ya Dkt. Hassan Abbas katika maelezo ya ukurasa wake mitandaoni ya kijamii (Profile) na kutuma jumbe kwa watu akiwaomba wamtumie fedha kwenye namba tofauti za simu.