
Mshatakiwa huyo amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Julai 30, mbele ya Hakimu Mkazi, Salum Ally.
Akisomewa mashtaka na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon amedai mshtakiwa ni mfanyabiashara ambaye anaishi maeneo ya Gezaulole Kigamboni Dar Es Salaam, na kwamba anatuhumiwa kumuua mkewe Mei 15, 2019.
Pamoja na kusomewa mashtaka hayo, mshtakiwa hakutakiwa kujibu lolote kwa sababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo, upelelezi wa kesi unaendelea na atarudishwa tena mahakamani hapo Agosti 13, ambapo kwa sasa amepelekwa gerezani.