Jumatano , 15th Jun , 2022

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya,  linamshikilia Warren Mwinuka (20),  mkazi wa Mtaa wa Makondeko jijini Mbeya kwa tuhuma za kujifanya ni Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera, akitumia akaunti ya mtandao wa kijamii wa Instagram  kwa jina la Mkuu huyo

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei

Kwa mujibu wa  Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya, Ulrich Matei amesema mtuhumiwa huyo alikamatwa  Juni 7 majira ya saa nane mchana  katika maeneo ya Mama John jijini Mbeya alipokuwa akiendelea kuwatapeli watu.

Akizungumzia tukio hilo, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera amelishukuru Jeshi la Polisi kitengo cha IT kwa jitihada za kufanikisha kumkamata mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akitumia akaunti yake kuwatapeli watu.

Aidha Homera amewasihi viongozi wenzake wakiwamo wanasiasi kujenga utamaduni wa kukagua mitandao yao ya kijamii.

Mtuhumiwa huyo Warren Mwinuka amekiri kufanya kitendo hicho