
Familiya ya mama Zena wakiwa nje ya nyumba yao maeneo ya Tegeta Namanga baada ya kubomolewa nyumba yao kutokana na kuwepo mgogoro wa ardhi
Akiongea na East Africa Radio Mama mjane Bi Zena Nassoro Mbwa wa familia hiyo amesema anakosa haki yake ya msingi kwa miaka mingi sasa kutokana na maafisa wa ardhi kushirikiana na mtu anayetaka kumtapeli kiwanja chake hivyo kuomba taasisi za kisheria kumsaidia kupata haki yake.
Akirejea kumbukumbu za hapo nyuma Bi Zena amesema miaka ya nyuma Mhe. John Magufuli akiwa waziri wa ardhi aliamuru arudishiwe kiwanja chake lakini wiki moja baadae baraza la mawaziri lilipo vunjwa maafisa ardhi walianza tena kumzungusha mpaka sasa.
Kwa sasa mama huyo na familia yake wakiwa na mtoto wa miezi 3 wanalala nje baada ya nyumba yao kuvunjwa na taasisi hiyo ya kibenki kwa madai ya kununua kiwanja hicho mwishoni mwa mwaka jana kutoka kwa Rashid Mandwanga aliyetumia ofa ya kiwanja hicho kutapeli eneo hilo.