Jumatatu , 20th Jun , 2016

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imezitaka jamii hasa familia zenye watu wenye ualbino kuhakikisha kuwa wanashirikim kiikamilifu kuendelea kukemea vitendo vyovyote vinavyoashiria kunyanyaswa kwa watu wenye ualbino nchini.

Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania imezitaka jamii haswa familia zenye watu wenye ualbino kuhakikisha kuwa wanashirikim kiikamilifu kuendelea kukemea vitendo vyovyote vinavyoashiria kunyanyaswa kwa watu wenye ualbino nchini.

Wito huo umetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora nchini Tanzania Tom Bahame Nyanduga wakati akieelezea maafikiano ya katika mkutano Afrika wa kimataifa wa mpango wa utekelezaji wa kuwalinda albino barani Afrika.

Akiongelea mikakati ya kuendelea kufanya ili kuwalinda watu wenye Ualbino barani Afrika mtaalamu huru wa umoja wa mataifa kwa watu wenye ualbino Ikponwasa Ero ameashauri familia zitakazofiwa na watu wenye ualbino wapewe saruji ili kujengea makaburi kuzuia kufukuliwa watu wenye ualbino , huku mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania Alvaro Rodriguez akisema wao kama Umoja wa Mataifa watasimamia albino wasiuwawe kama sera ya usawa.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa shirika lisilo la kiserikali linalowahudumia watu wenye Ualbino nchini Tanzania la Under the Same Sun Vicky Ntetema anasema kuwa watu wanaopita na watu wenye ualbino katika nchi moja kwenda nyingine wahojiwe na polisi wa kimataifa wa Interpol.