Jumatatu , 3rd Jan , 2022

Watu sita wameuawa hii leo Januari 3, 2022, katika shambulizi la kigaidi lililotokea katika Kijiji cha Widhu Majembeni kaunti ya Lamu nchini Kenya.

Al Shabab

Taarifa za polisi zinaarifu kuwa wanamgambo wa kundi la kigaidi la Al Shabab walivamia kijiji na kuchoma nyumba katika tukio la Jumatatu ya leo asubuhi.

Mwanakijiji mmoja alipigwa risasi hadi kufariki, wa pili alikatwakatwa hadi kufa na wengine wanne kuuawa kwa kuchomwa kwa moto.

Kamishna wa polisi kaunti ya Lamu Lamu Irungu Macharia, akithibitisha kutokea tukio hilo amesema uchunguzi zaidi unaendelea