Ijumaa , 29th Jul , 2016

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe, amesema kuwa akiba ya fedha za kigeni imeporomoka kutoka dola bilioni 4, za Marekani mwezi November Mwaka jana hadi kufikia dola bilioni 3.5 kufikia nusu ya kwanza mwaka huu.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo Zitto Kabwe.

Mhe. Zitto amesema kuwa alipata taarifa hizo alipokuwa akisoma ripoti ya Shirika la Fedha Duniani(IMF),jambo lililomfanya asome taarifa za benki kuu nchini Tanzania (BOT)na kubaini kushuka huko kwa fedha za kigeni.

Kiongozi huyo wa ACT- ambae pia ni Mtaaalamu wa uchumi amesema kuwa mwaka jana Tanzania ilikia na akiba ya dola bilioni nne ambazo zingetosha kuagidha bidhaa kwa miezi minne pekee.

Akitoa ufafanunuzi kuhusu suala hilo Gavana wa Benki kuu ya Tanzania, Prof. Beno Ndulu amesema hasi sasa akiba iliyopo ni bilioni 3.9 ambazo zinaweza kutumika zaidi ya miezi minne ijayo bila wasiwasi wowote.

Beno Ndulu amesema kuwa kilichochangia ni kushuka kwa beo ya mafuta ambayo ndiyo bidhaa iliyokuwa ikiingizwa zaidi hivyo kiasi cha mafuta kinachotumika kimeshuka.