Jumatano , 21st Sep , 2022

Maria Marwa (36) mkazi wa Kijiji cha Isango, wilayani Rorya mkoani Mara, amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa baada ya kujeruhiwa kwa mapanga na kukatwa mkono wa kushoto na titi la kushoto na mume wake kwa madai ya kukosekana kwa namba ya simu iliyopigwa kwenye simu ya mwanamke huyo.

Maria Marwa aliyekatwa mapanga

Akisimulia tukio hilo mwanamke huyo amesema usiku wa kuamkia Septemba 8 mwaka huu baada ya chakula cha usiku mume wake Werema Ibaso, alimuomba ampatie simu yake na kuanza kumhoji juu ya namba ya simu iliyopigwa siku mbili nyuma ambapo mwamke huyo alipoikosa ndipo mwanaume huyo alipochukua panga na kuanza kumkatakata maeneo mbalimbali ya mwili wake.

Akizungumzia sababu ya kukata mkono na titi Daktari wa hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Mara, amesema ngonjwa huyo alifika hospitalini hapo kwa kuchelewa hivyo majeraha aliyokuwa ameyapata yalianza kuharibika.

EATV ilimtafuta Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Tarime, Rorya Geofrey Sarakikya, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na amesema jeshi la polisi linaendelea kumsaka mwanaume huyo ambaye baada ya kufanya tukio hilo na kutoroka kusikojulikana.