Kaburi la Wilson Bahati
Akizungumza na #EastAfricaTV Grace Jeremia ambaye ni mke wa marehemu amesema kuwa, "Mume wangu alijinyonga kwa sababu alikosa hela ya kwenda msibani nyumbani kwetu ilikuwa saa 11:00 asubuhi aliniacha nimelala akavaa nguo akasema naenda shambani ndiyo tukamkuta sasa ameshajinyonga, tulikaa pamoja nyumbani tukazungumza lakini alisema hela amekosa sasa sijui alipata huzuni ndo akachukua uamuzi wa kujinyonga".
Kwa upande wake Baba wa marehemu amesema kuwa, "Nilikuwa sipo nyumbani nikapata taarifa mtoto wako amefariki nikauliza amefariki kivipi wakaniambia amefariki kwa kujinyonga, yaani nilisikitika sana nikatoka huko nyumbani nilipokuwa ninaishi nikaja nikafika hadi kwenye tukio nikaanza kujiuliza hivi kwanini mtoto wangu ajinyonge sijui ni kwa ajili ya majungu ya watoto wangu yaani nasikitika kwakweli,"
.Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo Afisa Mtendaji wa kijiji hicho amesema alitoa taarifa kituo cha polisi na askari walifika na kufanya uchunguzi wa tukio hilo na baadae familia ikaruhusiwa kuendelea na shughuli za mazishi.