Hayo yamebainishwa leo jijini Dar es salaam na waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano Prof Makame Mbarawa alipofanya kikao na menejimenti ya shirika hilo kwa lengo la kuwataka kujiandaa na mkakati huo.
''Tutawekeza kwenye Air Tanzania ili kuongeza fursa za kiuchumi pamoja na kuongeza wasafiri wengi watakaofika nchini pia kuinua sekta ya utalii'' Amesema waziri Mbarawa.
Aidha waziri amewakumbusha watendaji hao kuwa Rais yupo tayari kununua ndege mpya na kutoa mtaji kwa ajili ya shirika hilo ili liweze kushindana kimataifa.





