Ijumaa , 7th Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan, ameoneshwa kushangazwa na tabia ya vijana wengi nchini kwamba wakimaliza shule hukaa ndani na vyeti vyao wakisubiri ajira kutoka serikalini, badala ya kutafuta fursa za kazi ambazo zingewaingizia kipato.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 7, 2021, aliposhiriki maadhimisho ya kilele cha matembezi ya miaka 58 ya Mapinduzi matukufu ya Zanzibar, yaliyofanyika wilaya ya Mkoani, Kusini Pemba, huku akisisitiza kwamba ni jambo la aibu kwa kijana kukaa bila kazi kwa nchi kama Tanzania yenye fursa nyingi za kazi.

"Ni aibu kwa kijana kukaa bila kazi," amesema Rais Samia