Rais Mstaafu wa Afrika Kusini, Jacob Zuma
Mahakama ilikuwa na jukumu la kuamua kama Bw.Zuma anapaswa kuadhibiwa kwa kukataa wito wa mahakama na amri ya mahakama ya kumtaka afike mahakamani kutoa ushahidi kuhusu shutuma za rushwa wakati wa utawala wake.
Mwenyekiti wa kamati maalum ya uchunguzi wa Mahakama ,Raymond Zondo, ambayo imekuwa ikichunguza madai hayo aliiomba Mahakama hiyo itamke kuwa Rais huyo wa zamani aliidharau Mahakama na imhukumu kifungo cha miaka miwili.
Tangu alipojiuzulu mnamo mwaka 2018, Zuma amekuwa akifika mahakamani akikabiliwa na shutuma za ufisadi ambazo amekuwa akizikanusha.


