
Taarifa ya ICRC imeonya kuwa ukosefu wa chakula barani Afrika unatarajiwa kuwa mbaya zaidi kutokana na mizozo na ghasia za silaha, mavuno mabaya kwasababu ya ukame wa miaka mingi, na kuongezeka kwa bei ya chakula na bidhaa nyingine.
Imeeleza kuwa huenda watu wengi zaidi Barani afrika wakaingia kwenye baa la njaa na umaskini uliokithiri.
Tathmini ya hivi karibuni ya Umoja wa Mataifa inakadiria watu milioni 346 katika bara la afrika wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula, hii ikiwa na maana kwamba robo moja ya watu hawana chakula cha kutosha barani afrika
Mkurugenzi wa ICRC kanda ya Afrika, Patrick Youssef anasema hali ni ya dharura. huku akionya kuwa huenda maisha ya watu wengi yakapotea endapo hakutakuwa na juhudi za pamoja za wadau tofauti kukabiliana na changamoto zilizopo.
Youssef anasema pembe ya Afrika imeathirika zaidi huku maeneo mengine ya Afrika, kuanzia Mauritania hadi Sahel, mpaka Ziwa Chad na Jamhuri ya Afrika ya kati nayo yanakabiliwa na athari za mgogoro wa Ukraine.