Ijumaa , 9th Aug , 2024

Kijana aliyefahamika kwa jina la Shalom Tarimo (21) amefariki dunia leo Agosti 9, 2024, wakati akifanya usafi katika kituo cha mafuta cha Uhuru Peak mjini Moshi mkoani Kilimanjaro 

Kisima cha mafuta

Tarimo ambaye alikuwa kijana wa kazi amefariki dunia kwa kutumbukia kwenye kisima cha mafuta wakati akijaribu kuokota simu iliyomponyoka mfukoni.

Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifika na kuchukua takribani saa moja kutoa mwili wa marehemu katika kisima hicho kilichopo katika kituo cha mafuta cha Total Energies cha Uhuru Peak.