Afande Rama
Afande Rama ameachiwa huru hii leo baada ya Hakimu wa Mahakama hiyo Khamis Ali Simai kusema Mshtakiwa hana hatia na amemuachia huru kutokana na kifungu cha 220 cha sheria namba 7 ya mwaka 2018.
Kesi hiyo iliwasilishwa na Mwendesha Mashitaka kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka Mohamed Saleh ikiwa na jumla ya mashahidi 9 na wote wamewasilisha ushahidi ambao haukuweza kumtia hatiani mshtakiwa huyo.