Hayo yamesemwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi na Mawasiliano wa chama hicho, Ado Shaibu wakatu alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari leo, katika makao makuu ya ofisi zao zilizopo Sayansi Kijitonyma jirani na kanisa la KKKT Jijini Dar es Salaam.
"Tunawapongeza sana viongozi wetu wa dini kwa kujitokeza waziwazi kuonyesha ugandamizaji wa haki unaoendelea nchini. Hatua ya TEC kutoa waraka wa kiuchungaji ni kurasa mpya katika siasa zetu tangu uchaguzi mkuu wa mwaka 2015 ukamilike", amesema Shaibu.
Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC) lilitoa ujumbe huo siku za hivi karibuni ndani ya mwezi Februari ,2018 ambapo uliandikwa na maaskofu wote wa baraza hilo ikiwa ni maandalizi ya mfungo wa mwezi wa toba (kwaresma).
Kwa upande mwingine, Shaibu amewataka wananchi waendelee kuwaunga mkono chama hicho katika harakati za kuleta mabadiliko nchini ya kisiasa ili kuweza kubadili sera za uchumi wa nchi zifaidishe wananchi walio wengi.


