Jumatatu , 28th Sep , 2015

Mgombea Urais wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mngwira, amesema iwapo chama hicho kitapata ridhaa ya kuongoza nchi, kitahakikisha rasilimali za madini, gesi asilia na mafuta zinamilikiwa na wananchi kikatiba.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha ACT-Wazalendo, Anna Mngwira

Akizungumza leo katika mkutano wa kunadi sera za chama hicho uliofanyika katika uwanja wa Mashujaa mkoani Mtwara , amesema swala hilo tayari lipo katika ilani ya chama hicho na kwamba, wananchi ndio watakuwa na hati miliki ya rasilimali hizo za taifa.

Aidha Mama Mghwira ameongeza kuwa kwa utaratibu watakaouweka utamuwezesha mwananchi kumiliki rasirimali ya nchi yake kupitia serikali au kampuni yoyote binafsi au ya uma ili kuleta maendeleo ya kiuchumi kwa usawa.

Kwa upande wake, mgombea mwenza wa chama hicho, Hamad Yusuf, amesema miradi mbalimbali ya uwekezaji iliyopangwa kufanyika mjini Bagamoyo ikiwa ni pamoja na uwanja wa ndege na bandari, itafutwa na baadala yake uwekezaji huo utafanyika mkoani Mtwara.