
Mwanaume mmoja huko Marekani aliyetambulika kwa jina la Harrison Jones amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa sita ya jaribio la mauaji baada ya kudaiwa kuendesha gari zaidi ya kilomita 1100 ili kuchoma moto nyumba ya mwanaume mmoja wa Pennsylvania ambaye alikuwa akiwasiliana na mpenzi wake wa zamani, polisi wamesema.
Moto uliripotiwa katika nyumba ya Merganser Way huko Bensalem, Pennsylvania, muda wa saa 11 asubuhi tarehe 10 Februari, na kupelekea vikosi vya zimamoto kufika mahali hapo, kulingana na taarifa ya Idara ya Polisi ya Bensalem iliyotolewa Jumatatu.
Wapelelezi baadaye walibaini kuwa moto huo uliwashwa kwa makusudi, Picha za uchunguzi kutoka nyumba za jirani zilionyesha gari aina ya sedan nyeusi ikisimama karibu na makazi hayo saa 11 asubuhi, mtu mmoja alishuka kutoka kwenye gari akiwa amebeba kitu, akaelekea kwenye nyumba hiyo na kurudi kwenye gari hilo dakika 15 baadaye.
Muda mfupi baada ya mshukiwa kutoroka eneo hilo, mlipuko mkubwa uliteketeza nyumba hiyo kwa moto.
Wachunguzi walitumia kamera za makutano ya mji kufuatilia gari hiyo nyeusi yenye namba za usajili wa Michigan, ambayo iliwaongoza mpaka Michigan. Uchunguzi zaidi umebaini kuwa Harrison Jones, ambaye anaishi huko huko Michigan, alikuwa mpenzi wa zamani wa mwanamke ambaye alikuwa anawasiliana na Merganser Way anayeishi kwenye nyumba aliyochoma moto
Maafisa katika jimbo la Michigan walipata kibali cha kutafuta makazi ya Jones, ambapo waligundua vifaa vya kuvunja kufuri, simu ya mkononi, kompyuta na alama ya kuungua kwenye mkono wa Jones ambaye kwasasa amekamatwa na kushtakiwa kwa makosa sita ya jaribio la mauaji.