
Takwimu zinaonesha kuwa asilimia 60 ya watoto katika mikoa hiyo wana utapiamlo wa aina mbalimbali.
Akiongea katika hafla ya kutoa tuzo kwa wandishi wa habari za lishe nchini, Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Annastazia James Wambura amesema hali hiyo inachangiwa na mila na desturi ikiwa ni pamoja na watoto kupewa chakula mara tatu kwa siku sawa na watuwazima.
Mhe. Annastazia amesema, serikali itajikita zaidi kutekeleza malengo ya dunia na yale iliyojiwekea katika kuhakikisha kuwa wanapunguza udumavu wa watoto kwa asilimia 40, kupunguza idadi ya watoto wanaozaliwa na uzito pungufu kwa asilimia 30 na kudhibiti ukondefu wa watoto na kubakia asilimia 5 sambamba na kuongeza unyonyeshaji watoto kufikia asilimia 50 kwa mwaka 2015.
Naye, Mkurugenzi wa Jukwaa la Lishe nchini Tanzania PANITA Bwana Tumaini Mkindo amemwomba Rais Dkt. John Pombe Magufuli kuongeza hali ya utashi wa kisiasa miongoni mwa viongozi katika kushugulikia tatizo la lishe duni kwa kuzingatia kuwa madhara yake yana athari za kiafya, Kielimu, Uzalishaji na Ukuaji wa Uchumi.