Kipima joto
Hayo ni kwa mujibu wa Shirika la Hali ya Hewa Duniani (WMO), ambalo limesema barafu ya bahari ya Arctic iliyeyuka mapema na kwa kasi, ambayo ni ishara nyingine ya mabadiliko ya tabianchi.
Aidha, shirika hilo limesema kuwa viwango vya gesi ya mkaa, ambavyo vinachangia ongezeko la joto duniani, vilifikia upeo mpya.
Katibu Mkuu wa WMO, Petteri Taalas, amesema hali ya El Niño ya 2015/2016 imechangia viwango hivi vya joto.





