Wiki ya huduma kwa wateja EATV yakabidhi zawadi

Jumanne , 6th Oct , 2020

East Africa Television Limited kupitia kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio wamekabidhi kapu kutoka Royal Oven Bakery kwa ARiS Insurance wakiwa kama washindi wa shindano la kutafuta kitengo bora cha huduma kwa wateja.

Muandaaji wa kipindi cha SupaBreakfast cha East Africa Radio, Mackriner Siyovelwa (wa kwanza kushoto), akikabidhi zawadi kwa wafanyakazi wa ARiS Insurance.

Kampeni ya kutafuta wahudumu hao inaendeshwa kupitia wasikilizaji wao kuelezea namna ambavyo dawati la huduma kwa mteja katika taasisi husika ilivyosaidia kutatua tatizo lake.

Akizungumza baada ya kupatiwa kapu hilo mkuu wa kitengo cha huduma kwa wateja kutoka ARiS Insurance Winfrida Kawiche amesema kuwa mteja kwao ni mfalme na wamekuwa wakitoa huduma kwa hali ya upendo zaidi.

“Tunashukuru sana uongozi wa East Africa Television Limited, tunaahidi kuendeleza kile ambacho tunafanya maradufu ahsante pia kwa Royal Oven Bakery maana kapu limesheheni”, amesema Winfrida.