Alhamisi , 7th Oct , 2021

Application ya WhatsApp iko kwenye majaribio ya kuweka mfumo mpya wa kusikiliza ujumbe wa sauti (Voice Message/Notes) ambao utawezesha watumiaji kuendelea kusikiliza ujumbe huo hata ukiwa umefunga chat tofauti na ambayo ujumbe huo umetumwa.

Picha ya App ya WhatsApp

Mapinduzi haya ya Teknolojia yanakuja kurahisisha watumia wa App hii ambapo awali ilikuwa ukiifungua chat nyingine Voice Message inaacha ku-‘play’ na kukulazimu ubaki katika chat hiyo mpaka mwisho wa kusikiliza ujumbe.

Wakati unaundelea kusikiliza juu itatokea mstari wa rangi ambayo inafanana na Audio Player ambayo itaonyesha jina na profile ya aliyekutumia sauti (Voice Message/Notes).