Naibu spika wa baraza la wawakilishi, Mgeni Hassan
Akiongea kwa niaba ya Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, naibu spika wa baraza la wawakilishi, Mgeni Hassan kwenye hafla ya kufunga Mkutano wa kimataifa wa Madini, anasema, viwanda vitachochea nchi kufaidika na rasilimali.
“Wawekezaji wanatakiwa kuunga mkono Serikali katika kuongeza thamani Madini nchini, ili nchi inufaike ipasavyo na uwepo wa rasilimali hizo mpaka kufikia uzalishaji wa bidhaa”, Mgeni Hassan, Naibu Spika baraza la wawakilishi.
“Ilifanyika tafiti kwenye Kisiwa cha Pemba, na kumegundulika Madini ya vifaa Vya ujenzi, simu, betri pamoja na ndege, hivyo niwakaribishe wawekezaji kukimbilia fursa hii kuwekeza kwenye visiwa hivyo”, Antony Mavunde, Waziri wa Madini.
Baadhi ya wachimbaji wameomba Serikali kuwawezesha vifaa pamoja na mitaji ili waweze kufanikiwa.
“Wachimbaji wengi hatuna mitaji na kitu tunachojitaji hapa sio Pesa bali ni vifaa Vya uchimbaji ili tufanye uzalishaji wenye tija”, Raenatus Kapila, Mchimbaji Madini ya Bati.
“Wachimbaji wadogo tunasbuliwa na wamiliki wa maeneo kuna muda tunashindwa kufanya uzalishaji kwa sababu wamiliki wa Ardhi wanataka zaidi ya tunachowekeza”, Kuruthum Issa, Mchimbaji Madini ya Nikel.