Jumatano , 19th Oct , 2022

Wavuvi zaidi ya 6,000 katika mkoa wa Kagera, wanatarajiwa kunufaika na mikopo ambayo itatolewa na serikali kwa lengo la kupunguza tatizo la ajira hasa kwa vijana, ambao wamekuwa wakifanya shughuli hizo kwa kusuasua kutokana na kutokuwa mitaji na zana bora za uvuvi. 

Afisa uvuvi wa mkoa wa Kagera Ephraz Mkama amesema mikopo hiyo ni kwa ajili ya kunua zana bora za kuendesha shughuli zao pamoja na ufugaji wa samaki katika vizimba.

"Katika mkoa wa Kagera serikali tayari imebainisha maeneo yanayofaa kwa ufugaji wa samaki, tulipata maeneo kama sita yakiwamo ya Rubafu, Nyamkazi, Kifungwa na Makongo, yote haya yamebainika yanafaa na yana mazingira mazuri yanayofaa katika ufugaji wa samaki na ukuaji wa samaki" amesema Mkama.

Kwa upande wake Afisa Mwandamizi kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi makao makuu Dodoma, Clemence Katunzi amesema kuwa mikopo hiyo isiyo na riba inatolewa kwa vyama vya ushirika vya wavuvi, vikundi vya uvuvi vilivyosajiliwa na idara ya Maendeleo ya Jamii, makampuni ya watu binafsi yanayofanya shughuli za uvuvi na watu binafsi wanaofanya shughuli hizo, na kwamba wameingia makubaliano na benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania -TADB- kwa ajili ya ufuatiliaji wa mikopo hiyo.