Alhamisi , 2nd Mar , 2023

Ofisi ya Wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza imesema wafanyabiashara na wasambazaji wa gesi watakaofanya udanganyifu kwenye mizani ya kupima uzito wa mitungi ya gesi watapigwa faini isiyozidi shilingi milioni 20.

Mitungi ya gesi

Onyo hilo limetolewa na Meneja wa Wakala wa Vipimo mkoa wa Mwanza Hilolimus Mahundi, katika kikao cha kuwajengea uelewa wadau wa biashara ya gesi ili waweze kuzingatia matumizi sahihi ya vipimo kwa ajili ya kumlinda mlaji wa mwisho asipate kipimo pungufu katika mitungi ya gesi.