
Mapema hii Leo taasisi za kifedha,madalali na Watalaamu kutoka masoko ya mitaji wamekutana Kwa pamoja kujadili mfuko huo wa pamoja wenye lengo la kuanza kuuza vipande Nov mosi mwaka 2022.
Akizungumza namna mfuko huo utakavyofanya kazi na faida zake Kwa wateja amesema Dr Fred Msemwa amesema ni muda mwafaka sasa Kwa Watanzania kujitokeza kuwekeza Kwa muda mfupi na mrefu kupitia hati fungani.
"Watu wengi saizi wanashindwa kuwekeza moja kwa mojam kwenye mifuko kwa kuwa na kiasi kidogo cha fedha lakini kupitia mfuko huu sasa wataweza kuwekeza kwa pamoja na kukuza mitaji na kununua vipande"amesema Dr Fred Msemwa-Mkurugenzi mtendaji Watumisho Housing.
Uwekezaji huo unaweza kufanyika Kwa Njia ya Simu janja na ukiwa tayari umewekea misingi Kwa nchi nzima ukipangwa kusimamiwa na kuratibiwa na benki ya CRDB benki.
Kwa takribani Miezi miwili ya kwanza wawekezaji wote watagawiwa mapato yote ya uwekezaji bila makato yeyote na kwamba vipande vitanzaa kuuzwa mwezi wa Tatu.