Jumanne , 2nd Aug , 2022

Watafiti Nguli nchini Tanzania wasema kwa sasa nchi inatakiwa kuzidi kuongeza viwanda vingi ili kuongeza thamani ya rasilimali za asilia nyingi zinazopatikana kwenye mikoa mbalimbali ikiwemo gesi asilia, madini, Kilimo, pamoja na mafuta ili kukuza uchumi wa Taifa.

Tafiti zinaonesha kuwa wachimbaji wadogo wa madini bado hawajaweza kunufaika kwenye sekta hiyo kutokana na kuuza madini ambayo hayajaongezewa thamani hali ambayo sasa imewaketisha pamoja watafiti Nguli kutoka Taasisi ya Repoa kutoa mafunzo Kwa wadau wa kutoka mashirika mbalimbali kuzitazama sera na namna gani kama nchi inaweza kunufaika na rasilimali za asilia.

Hata hivyo Dk Peter Kafumu  aliyewahi kuwa Kamishna wa madini nchini amesema ugumu wa sera unatokana katika kuweka mzani sawa kati ya wawekezaji wanaokuja pamoja na wananchi Kwa pamoja kuweza kunufaika na rasilimali ambazo zinatajwa kuisha endapo mipango thabiti itachelewa.

Kwa upande wao washiriki mafunzo hayo wamesema uwekezaji unatakiwa katika teknolojia,ushirikishwaji wa wananchi na watunga sera Hali itakayoondosha mikataba mibovu iliyokuwepo hali  itakayoongeza ajira.
Ili uchumi ukuwe watafiti wanashauri lazima sera ziwe Shirikishi Kwa rasilimali zinaisha.