Jumatano , 15th Mar , 2023

Mstahiki meya wa Kinondoni Songoro Mnyonge amewataka wadada waliokuwa wakifanya biashara ya kuuza miili yao kupitia madungulo kujiandikisha majina yao kupitia serikali za mitaa wanayotoka ili kuwabaini rasmi kwa ajili ya kupatiwa mikopo.

Msitahiki meya wa Kinondoni Songoro Mnyonge

Utakumbuka siku chache Meya huyu aliibuka na sakata la wadada wanafanya biashara hiyo eneo la minazini kata ya makumbusho na kutoa maagizo moja ikiwataka wamiliki wa nyumba hizo kujisalimisha  na pia wadada hao kufika ofisini kwake ili wapatiwe mikopo waachane na biashara hiyo...

Hii leo nimefika kujua hatma ya tamko lile huku mstahiki meya akibainisha kuwa watu walijazana ofisini wengine hata wakiwa sio sehemu ya wadada wale na kuamua sasa kuwarejesha wote waanzie kwenye serikali zao za mitaa ili kuwabaini kila mmoja wapi anatokea...

Sambamba na hilo Meya huyo amewataka wale wote wenye vituo vya kufanyia watu massage na havijasajiliwa wala kuwa na leseni wajisalimishe mara moja, kwani kufanya hivyo wanaikosesha serikali mapato.

Aidha Mnyonge ameyasema hayo kufuatia operesheni iliyofanyika kimyakimya na kubaini uwepo wa nyumba nyingi zinazofanya huduma ya massage na matendo ya ngono zembe.

Licha ya jitihada za kuzitafuta baadhi ya nyumba hizo za Massage kusema na watoa huduma hiyo lakini ushirikiano umekuwa hafifu wengi hawakutaka kurekodiwa