Jumatano , 14th Dec , 2022

Naibu Wizara ya Viwanda Biashara na Uwekezaji imewataka watanzania kuchangamkia fursa za uzalishaji wa malighafi ili kukidhi mahitaji ya viwanda vinavyojengwa nchini.

Naibu Waziri wa Viwanda, Exaud Kigahe akitembelea mabanda katika maonesho ya vifaa tiba jijini Dar es Salaam.

Naibu Waziri wa Uwekezaji Exaud Kigahe, wakati akitembelea mabanda mbalimbali katika maonesho ya vifaa tiba jijini Dar es Salaam, amebainisha kuwa kwa sasa serikali imejikita katika kuweka mazingira bora kwa wawekezaji kutoka sekta binafsi.

Aidha Naibu Waziri Kigahe amewahakikishia wakezaji kwenye vifaa tiba, masoko ya vifaa watakavyovizalisha ikiwa pamoja na soko la uhakika kutoka serikalini.

Kwa upande wao Mamlaka ya uwekezaji wa maeneo maalum EPZA wamebainisha kuwa maonesho haya yatasaidia katika kuongeza idadi ya wawezaji nchini, huku baadhi ya wawekezaji hao wakikiri kuridhishwa na mazingira ya uwekezaji nchini.

Maonesho hayo yameanza leo, na yanatarajiwa kusiha Disemba 16, 2022 katika ukumbi wa Diamond Jubilee.