Jumatatu , 8th Aug , 2022

Wakulima wa Kanda ya Kaskazini wametakiwa kuendana  mabadiliko ya Teknolojia katika  kilimo hususani  kwenye matumizi ya pembejeo bora za kilimo  Ili kupata mazao yenye tija kwa taifa.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha wa John Mongella

Mkuu wa Mkoa wa Manyara  Makongoro Nyerere ana tumia nafasi hiyo kupenyeza neno kwa wakulima kuelekeza nguvu yakutafuta mbinu mpya za kufanya kilimo cha kisasa ili kusaidia kupata mavuno yanayotosholeza  mahitaji hapa nchini.  

Kwa upande wake  Mkuu wa Mkoa wa Arusha wa John Mongella  anabainisha mikakati ya serikali ya kuyaongezea thamani maonyesho hayo yawe na hadhi ya kimataifa kwa msimu ujao.  

   
Baadhi ya wakulima walioshiriki maonyesho hayo wanaona ipo haja ya kuboreshwa  kwa maonyesho kutokana na umuhimu wake wa kusaidia katika sekta ya kilimo hususani suala la mbegu.