Ijumaa , 30th Jun , 2023

Serikali ya Tanzania Kwa kushirikiana na nchi ya Denmark imesema hadi sasa matarajio ya uanzishwaji wa asasi ya Pass trust kwa lengo la kuondoa changamoto ya Wakulima hasa wadogo ambao hawana dhamana ya sheria ya fedha kama inavyohitaji imefikiwa kwa kiasi kikubwa.

Akitoa taarifa hiyo Mkurugenzi wa biashara kutoka Pass Trust Adam Kamanda katika maadhimisho ya siku ya Ushirika Duniani ambapo kitaifa amesema kuwa kutokana na kuwepo Kwa changamoto dhidi ya Wakulima Serikali ya Tanzania na Denmark ikaanzisha Pass Trust kama mfuko ambao uko chini ya Ofisi ya Waziri mkuu.

"Kwa kifupi lengo la mfuko huu na kazi yake ni kutathmini biashara, kutengeneza Mpango Biashara katika sekta ya kilimo kuanzia wavuvi, wafugaji, wa samaki,wakulima wadogo Kwa wakubwa kuwatengenezea mpango biashara kufanya tathimini na kuchukua mipango biashara hiyo kuiwekea dhamana."amesema

Kamanda amefafanua kuwa dhamana hiyo inatolewa mpaka asilimia 60 Kwa jamii nzima lakini inatoa mpaka asilimia 80 Kwa miradi yote ambayo inahusisha wanawake, Vijana au inafanya kilimo kinachozingatia utunzaji wa mazingira na kuongeza kuwa katika hilo wanawake na vijana mara nyingi hawana dhamana

Amesema kuwa mpaka hivi sasa pass trust imeweza kufanya biashara Zaidi ya 66,000 na imeweza kutoa mikopo kwenye dhamana inayozidi takribani tirioni 1.5 mpaka Sasa hiyo ni karibu asilimia 25 ya mikopo yote ya kilimo inadhamana ya pass trust.

Serikali ya Tanzania na Dennymark imeshukuliwa na wakulima kwa kubuni mfuko huo kwa sababu umechochea sehemu kubwa ya sekta hiyo ya kilimo,huku baadhi ya wanufaika wa mfuko huo wakieleza hali ilivyo kuwa kabla ya uanzishwaji wa mfuko huo kupitia ofisi ya waziri mkuu