Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Changamoto ya Masoko inayowakabili wakulima kwa nyakati tofauti za mavuvo ya mazao yao zimeelezwa kuchangiwa na wakulima kutoendana na wakati wa kutumia  teknolojia hivyo utafutaji wa masoko kigitali umetajwa kuwa mwarobaini wa kumkwamua mkulima kimasoko

Hayo yamebainishwa na Taasisi   ya Taarifa ya Masoko  Kigitaki AGROMOVIL Baada ya Kukutana na Umoja wa Wakulima wa Zao la Parachichi NSHDA yenye wakulima zaidi ya Elfu Tano na Kuwataka Wakulima Hao Kutumia Teknolojia ya Kisasa Kwani Humsadia Hata Mkulima Kutuna Kumbukumbu zake

Mkurugenzi Asasi ya wakulima  mkoa wa Njombe na  Bwanashamba kutoka Taasisi ya Maendeleo  ya mazao ya Mboga, Matunda na Viungo (TAHA)  wanasema mfumo wa masoko ya kidigitali utaondoa madalali wanao tarajia kutengeneza faida.

Baadhi ya Washiriki wa Mafunzo hayo wamesema mfumo huo utawaongezea  tija katika kilimo wanachokifanya.