
Wafanyabiashara wa tikiti
Wakizungumza na EATV leo Novemba 24, 2022, wafanyabiashara hao wa tikiti wameonyesha kutoridhishwa kuondoka katika eneo hilo kwa kile walichodai kwamba soko hilo limekuwa ni soko kubwa katika nchi za Afrika Mashariki na na hivyo wameiomba serikali kuliangalia suala hilo kwa jicho la huruma
Akizungumzia hatua hiyo Makamu Mwenyekiti wa soko hilo Omari Mbwana, amesema atakayeathirika zaidi ni mfanyabiashara na mkulima kwa kuwa tikiti zinazolimwa nchi nzima zinaletwa katika soko hilo hivyo itawachukua muda kupata soko ambalo litazoeleka kama lilivyokuwa soko la Tazara veternary.
Kwa upande wake Kaimu Mkuu wa idara ya viwanda, biashara na uwekezaji kutoka Manispaa ya Temeke Ramadhani Gurumukwa, amekiri kuwepo kwa taarifa za kutaka kuondolewa kwa wafanyabiashara hao na kwamba kwa sasa wameshaanza jitihada za kuwapatia masoko mengine ambayo watatumia wafanyabiashara wa tikiti kufanya biashara zao za tikiti maji.