Jumatano , 16th Nov , 2022

Kufuatia usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wateja na wafanyabiashara wanaolipa kodi,malipo mbalimbali ya serikali na wanaolipia mizigo yao bandarini serikali kupitia benki ya biashara ya Taifa TCB imefungua Tawi maalum eneo la bandari ambalo litafanya kazi saa 24 siku saba za wiki.

Hatua hiyo imefikiwa kufuatia malalamiko na usumbufu ambao wamekuwa wakiupata wafanyabiashara hasa wanaolipia merejesho ya ongezeko la thamani VAT ambao wengi wao wamekuwa wakikumbwa na kulipa penati kutokana na maeneo mengi ya taasisi za kifedha kufunga mapema huku wafanyabiashara hao wakielezea hali ilivyokuwa huko nyuma.

'hili tawi la benki ya biashara ya taifa kwa hapa badari limelenga kuwasaidia watanzania wote kuleta urahisi zaidi kweny ulipaji wa mapato mbalimbali ya serikali lakini pia litawasaidia wanaolipia marejesho ya kodi za mwaka kuepuka penati kwa kuwa litakuwa likifanya kazi saa 24 siku saba za wiki na sisi tuko tayari tumajipanga kutoa huduma hiyo' amesema Sabasaba Moshingi Afisa mtandaji Mkuu wa Benki ya Biashra ya Taifa.TCB

Tawi hilo maalum la bandari sasa litawapa nafuu wateja watumishi na hasa wafanyabiashara kufanya malipo huku pia pakiwekwa fursa ya wateja kupata mikopo kwa ajili ya kukuza biashara zao.

Takribani tawi hilo la bandari limeshakusanya zaidi ya shilingi bilioni 50 hivyo kuwa nauhakika wa kuwahudumia wafanyabiashara wa nyaja zote.