Jumatano , 16th Nov , 2022

Kampuni ya Vodacom Tanzania Plc imezindua vipanga njia (Routers) vya 5G ambavyo vitaunganisha nyumba na biashara kwenye mtandao wa 5G unaounganisha wateja kwa haraka na urahisi zaidi. 

Mnamo mwezi Septemba, Vodacom Tanzania ilizindua mtandao wa kwanza wa 5G nchini, kuashiria hatua kubwa ya maendeleo katika uvumbuzi na teknolojia. Kupitia 5G, wateja sio tu watafaidika na kasi ya haraka na yenye utulivu bali pia watanufaika na matumizi ya teknolojia zinazoibuka kama vile matumizi ya Intaneti na akili bandia

Hivi karibuni mara baada ya kununua mawanda imepanga kuyatumia kupanua mtandao na uwekezaji, ikijumuisha usambazaji wa mtandao wenye kasi wa 5G.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Mkurugenzi wa Vodacom Business, Arjun Dhillon alisema, “pamoja na kwamba 5G imezinduliwa nchini, bado haijaanza kutumiwa na wateja wetu na wafanyabiashara wengi kutokana na ukweli kwamba vifaa vingi vya intaneti vinakosa uwezo wa kuunganishwa kwenye 5G, kwa hivyo leo tunafurahia kuzindua vipanga njia vyetu vya 5G ambavyo vitawezesha wateja wetu kufurahia intaneti yenye kasi ya 5G.”

Kupitia uwepo wa 5G, wafanyabiashara na wateja wa kampuni hiyo watapata nafasi ya kutumia intaneti yenye uwezo mkubwa zaidi, na muda mchache wa kusubiri ambao utasaidia ubunifu zaidi na hivyo kujenga Tanzania iliyo bora na iliyounganishwa na dunia nzima.

Kwa sasa, mtandao wa 5G unapatikana Dar es salaam pekee huku kukiwa na mipango ya kupanua teknolojia ya 5G hadi takriban maeneo 230 nchini, yakiwemo Arusha, Dodoma, Mwanza, Iringa, Kagera, Zanzibar na Mbeya