
Mkuu wa Kitengo cha Masoko Vodacom Nandi Mwiyombella
Akizungumza na waandishi wa habari, Mkuu wa Kitengo cha Masoko Vodacom Nandi Mwiyombella amesema nia ya kampuni hiyo ni kuipeleka Tanzania katika ulimwengu wa kidijitali zaidi.
"Umuhimu wa mtandao wenye kasi kwa kila mtumiaji wa smartphone unajulikana na ili watanzania tusiwe nyuma na ukuaji wa teknolojia tunahitaji mtandao wenye kasi ili kujifunza Mambo mapya"amesema Nandi Mwiyombella
''Kwa kuzingatia hilo Vodacom Tanzania inakusogeza karibu na ulimwengu wa kidijitali kupitia ofa ya GB 96 katika kila simu ya Infinix NOTE 8 kwa muda wa mwaka mzima"ameongeza Nandy Mwiyombella
Naye Afisa mahusiano wa Infinix Aisha Karupa amesema simu hiyo mpya inauwezo kuhimili application zenye uwezo mkubwa pasipo simu kupata Moto au kuzima ghafla wakati wa matumizi.