Jumanne , 18th Oct , 2022

TRA mkoa wa Geita, imeendelea kutoa semina kwa wafanyabiashara wilayani Nyang'hwale juu ya umuhimu wa kurasimisha biashara zao na kujisajili kupata TIN, kutunza kumbukumbu na kutumia mashine za EFD na kutoa risiti ili kuepusha malalamiko wanapokuja kufanyiwa tathmini ya ulipaji wa kodi.

Wafanyabiashara wilayani Nyang'hwale, wakipewa elimu

Akitoa elimu kwa wafanyabiashara hao, Afisa Elimu na huduma kwa mlipakodi mkoa wa Geita Justine Katiti, amesema wafanyabiashara wengi wamekuwa wakikosa fursa za kufanya biashara  na wadau mbalimbali kwa kuwa hawajajisajili TRA, pia kutojisajili kumewakosesha fursa za mikopo kwenye taasisi za fedha.

"Wafanyabiashara tukiweka kumbukumbu sahihi za biashara zetu na kutoa risiti kwa kila mauzo tunayofanya tutakadiriwa na kulipa kodi stahiki, tutaondoa malalamiko ya kodi, biashara zetu zitazidi kupanuka na serikali itakusanya mapato yake na hivyo kutoa huduma bora zaidi na haraka kwa wananchi wake," amesema Katiti