Jumanne , 29th Nov , 2022

Mwanzoni mwa Mwaka 2023  serikali ya Uingereza imetangaza ku-wa na mpango maalum kwa kuondoa ushuru kwenye bidhaa zinazotoka Tanzania ili kuongeza ushindani kwa masoko ya bidhaa hizo nchini Uingereza.

Balozi wa Uingereza Tanzania Bwana David Concar pamoja na Mwakilishi maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwenye masuala ya Biashara Tanzania Lord Walney.

Hayo yamebainishwa katika Kongamano la pili kati ya Tanzania na Uingereza wenye lengo la kuwaleta pamoja wafanyabiashara na wawekezaji wa Tanzania na Uingereza.

Naibu katibu Mkuu wa Wizara ya Uwekezaji Ally gugu ameongeza kuwa pia wataweka vigezo rahisi ambavyo vitakuwa sio changamoto kwa wafanyabiashara wa Tanzania kupeleka bidhaa zao Uingereza.

Kwa upande wa Uingereza, Bwana David Concar ambaye ni Balozi wa Uingereza Tanzania, ameahidi kuwa wataendelea kuongeza ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, hasa kwenye masuala ya biashara na uwekezaji huku Mwakilishi maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza kwenye masuala ya Biashara Tanzania Lord Walney akibaibisha kuwa wataendelea kushirikiana na nchi zinazoendelea katika kukuza uchumi.

Katika kongamano la mwaka jana makampuni zaidi ya 10 kutoka Uingereza, na mwaka huu wagenu kutoka Uingereza zaidi ya 30 wamehudhuria mkutano huo.