
Rais wa Shirikisho la vyama vya wachimbaji wa madini Tanzania (FEMATA), John Bina.
Rais huyo amesema hayo leo Septemba 22,2020 wakati akitembelea banda la Tume ya madini katika maonesho ya teknolojia yanayoendelea katika Kiwanja vya uwekezaji cha bomba mbili mjini Geita.
Aidha amepongeza kazi kubwa inayofanywa na Tume ya Madini kwenye usimamizi wa Sekta hiyo na kudai kuwa itaongeza uwekezaji katika madini.
Hata hivyo Bw.Bina amesema maendeleo ya Tume ya Madini yanayoonekana kwa sasa yanasaidia kukuza sekta ya madini na uchumi kwa ujumla.