Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

TRA Geita yaombwa kuwatazama wachimbaji wadogo

Jumamosi , 26th Nov , 2022

Mkuu wa Mkoa wa Geita Martine Shigella ameiomba mamlaka ya mapato Tanzania (TRA) mkoani humo kushirikiana na wizara ya madini pamoja na wizara ya Fedha kufanya Tathmini ya pamoja  ili waweze kuja na mapendekezo sahihi ya ukadiriaji wa kodi kwa wachimbaji wadogo

Shigela ameyasema hayo wakati kwenye maadhimisho ya siku ya shujrani kwa mlipa kodi iliyoambatana na utoaji wa vyeti kwa walipa kodi mkoani humo. 

"Unafanya uzoefu wa miaka hata mitano kwamba kwenye kipengele hiki tulikadiria kukusanya kiasi hiki kutoka kwa watu wa Madini kama sehemu ya 30% ya income tax, lakini mwaka juzi tukikusanya hiki, mwaka Jana tumekusanya hiki,  kwahiyo mnatafuta ratio ambayo itawasaidia kwenye kodi ili hiyo percent isiwe kubwa sana ikaleta malalamiko au ikawa ndogo sana inaonekana mmecompromise katika ukusanyaji wa kodi, tukifanya hivyo kazi yetu itakuwa nyepesi", alisema Shigela. 

Kaimu kamishna wa TRA nchini anasema katika kipindincha miezi minne wamefanikiwa kukusanya mapato kwa asilimia 208.

"Katika kipindi cha mwezi Julai 2022 hadi oktoba 2022, mkoa wa Geita uliweza kukusanya shilingi bilioni 25.27 ikiwa ni ufanisi wa asilimia  208.6 dhidi ya lengo la kukusanya shilingi bilioni 12.11 katika kipindi hiko ", alisema 
Baadhi ya wafanyabiashara mkoani humo wameiomba TRA iendelee kutoa Elimu kwa wafanyabiashara ili kuondoa malalamiko wakati wa ukusanyaji wa kodi huku wengine wakiipongeza kwa huduma za kielektroniki. 

"Tunaomba wenzetu wa TRA, waendelee kuandaa Elimu kwetu sisi wafanyabiashara ili tuendelee kuoata Elimu ya kutosha hasa ukizingatia kwamba wengi bado Elimu haijatosha, kwahiyo tuendelee kuoata Elimu ili tuweze kuwa free kulipa kodi sisi wenyewe bila kufosiwa", alisema Wambura. 

"Kaka sasa hivi  unaweza, ukaingia kwenye mtandao shughuli zako zote ukazituma kwa njia ya mtandao bila kusumbuka kwenda ofisi za TRA hiyo ni namna fulani wameiboresha wao kwa ajili ya ulipaji wa kodi", alisema Inyasi. 

HABARI ZAIDI

Rajab Abrahaman Abdalah, Mwenyekiti wa CCM Mkoa Tanga

CCM Tanga yaijibu CHADEMA kuhusu huduma za kijamii

Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) Jenista Mhagama

Wazazi simamieni maadili kwa watoto 

Sehemu ya Ardhi iliyoathirika na Mabadiliko ya Tabia Nchi

Hizi hapa sababu za hali ya hewa isiyotarajiwa

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu