Alhamisi , 17th Mar , 2022

Mkurugenzi wa Biashara kutoka Tanzania Distilleries (TDL) Limited wazalishaji wa Konyagi, Timea Chogo, amesema kwamba kampuni hiyo kwa mwaka huu imepanga kununua tani 1,500 za zabibu kutoka kwa wakulima wanawake wa zao hilo.

Mkurugenzi wa Biashara kutoka Tanzania Distilleries (TDL) Limited wazalishaji wa Konyagi, Timea Chogo

Kauli hiyo ameitoa hii leo Machi 17, 2022, wakati akizungumza kwenye kipindi cha Supa Breakfast cha East Africa Radio, ambapo amesema kwamba katika mwaka 2021 walinunua tani 233 za zabibu kwa ajili ya kutengeneza mchuzi wa Dodoma Wine".

"Mwaka huu tunategemea kwamba tutanunua kama tani 1,500 na lengo letu kubwa ni kuwawezesha wanawake ambao wapo katika kilimo cha zabibu yaani grapes farmers kwa angalau asilimia 40 ili tuwasaidie na wao kukua," amesema Timea Chogo.

Timea Chogo ameongeza kwa kusema kuwa, "Programu yetu kubwa ukiachana na Konyagi tunazalisha pia Dodoma Wine, tunafanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakulima wa zabibu, 2021 tulinunua tani 233 za zabibu kwa ajili ya kutengeneza mchuzi wa Dodoma Wine".