Jumatano , 21st Sep , 2022

Wakulima na wadau wa Kilimo mkoani Morogoro wameiomba serikali kuangalia upya suala la kufungua mipaka ya nchi ambalo limepelekea wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuingia nchini na kununua mazao yakiwa mashambani na mashineni licha ya kuwepo na mavuno machache kwenye msimu uliyopita.

Mazao ya chakula na biashara

Hali hiyo imetajwa kusababisha kuwepo kwa mfumuko wa bei za mazao ya nafaka ikiwemo mahindi, mchele pamoja na mazao mengine  hapa nchini kutokana na kuwepo kwa upungufu wa mazao hayo.

Wakizungumzia hali hiyo mkoani humo  ambayo kwa sasa wanadai imepekea mazao ya chakula kupanda seikali ina kila sababu za kuingilia kati ili kunufaisha wafanyabiashara wa ndani.

Kwa upande wao baadhi ya wadau wa kilimo mkoani Morogoro, wameeleza athari za kupanda kwa bei za mazao na kuishauri serikali kuhusu kufunguliwa kwa mipaka ambayo imepelekea wafanyabiashara kutoka nje ya nchi kuja Tanzania kuchukua mazao ya chakula.