Jumanne , 2nd Mei , 2023

Serikali yakutana na wakuu wa mashirikia ya umma saba ya kimkakati na wabobezi wa uwekezaji wa ubia ya sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuvutia mitaji ya kiasi cha dola za kimarekani Bilioni 9 sawa na shilingi trilioni 21 ndani ya miaka mitano

 

Akizungumza katika warsha hiyo Kamishina wa Ubia ya sekta ya Umma na sekta binafsi (PPP) David Kafulila amesema kuwa hatua hiyo ya kukutana na mashirika hayo yenye lengo la kujadili sekta mbili ikiwemo sekta ya miundombinu ya umeme pamoja na sekta ya uchukuzi inatazamiwa kuleta chachu ya kukamilisha miradi mbalimbali ya ubia nchini.

Aidha, Kafulila amebainisha kuwa wapo katika hatua ya kutafuta muwekezaji kwaajili ya ujenzi wa barabara kati ya kibaha mpaka morogoro , ikiwa na mgawanyo wa sehemu mbili ya ujenzi huo.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Mipango Jenifa Omolo amebainisha kuwa hatua ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo inatarajiwa kujenga katika mradi huo wa ubia utaweza kuchangia na kunufaisha sekta mbalimbali ikiwemo kilimo na kusaidia wakulima kusafirisha mazao yao kwa muda mfupi tofauti na kutumia muda mwingi katika usafirishaji wa mazao hayo.