
Mavunde amesema hayo katika jukwaa la kilimo kwa ukanda wa Afrika mashariki na kusini mwa Afrika ambapo Tanzania ni mwenyeji wa mkutano huo ulioanza leo jijini Dar es salaam huku serikali ikipanga kununua ndege ya kumwagilia dawa mashambani
Mavunde amesema takribani mabonde 22 yote utekelezaji umeanza nchi nzima ikiwa ni jitihada za kupambana na ukame pamoja na mabadiliko ya Tabia nchi
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Sacau ambao hujumuisha ukanda wa nchi za SADEC Dkt Sanare amesema mkutano huo umewakutanisha wafadhili kwenye sekta ya kilimo ili kurekebisha sekta ya Kilimo hususani kwa vijana ambao ndio walengwa