Jumatatu , 25th Apr , 2022

Naibu Spika wa Bunge la Tanzania  Mussa Azan Zungu amezipongeza taasisi za kifedha nchini kwa kuunga mkono harakati za serikali katika kuwajengea wananchi uwezo wa kiuchumi, ikiwa ni pamoja na kutoa mikopo kwa wajasiriamali wanaoanzisha miradi mbalimbali ili kujiletea maendeleo

Kauli ameitoa wakati akizungumza kwenye hafla ya futari iliyoandaliwa na BancABC jijini Dar es Salaam kwa ajili ya wateja wake wakati huu ambao waumini wa dini ya kiislam wanatekeleza moja ya nguzo muhimu kwa kufunga mwezi mtukufu wa Ramadhani.

“Hatua ya kuwawezesha wajasiriamali ni kumuunga mkono Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye wakati wote amehakikisha vikwazo vya kibiashara kwa kundi hilo vinaondoka ikiwa ni pamoja na kuwawekea mazingira bora ya kufanya biashara zao,hivyo ni kwenu sasa kama wawekezaji kutumia nafasi hiyo kufanya biashara Tanzania”alisema Mussa Zungu - Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

 Awali Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Imani John alieleza kuwa ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yake hapa nchini unatokana na namna serikali ya Tanzania ilivyoweka mfumo imara kwa taasisi za fedha kutekeleza majukumu yao, hatua ambayo imeongeza kasi ya jamii kutumia huduma za kibenki.

 “kiukweli nime mkweli uwekezaji na kasi tulyo nayo kama benkABC inatokana na sera za nchi na utayari wa taifa kuwek misingi kwa wawekezaji hususani katika sekt6a bionafsi kwenye taasisi za kifedha.”alisema Imani sambamba na Jasmini Tuly mmoja ya wateja wa bankABC kwa kipindi kirefu.