
Pichani: kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko John Maige.
Ujumbe huo umetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa bodi ya nafaka na mazao mchanganyiko John Maige wakati wa hafla ya kusaini mkataba wa makubaliano na Kampuni ya KPMG Kwa lengo ya kuandaa mpango makakati wa awamu ya pili wa kutanua wigo wa kuuza nafaka zaidi ndani na nje ya nchi.
Amesema Wakulima wanatakiwa kuyatumia maghala ya kihifadhia nafaka yaliyo katika kanda Tano za kilimo ili kuwa na uhakika wa kutunza mazao yao katika hali ya usalama Ameongeza kuwa katika mpango mkakati wa awamu ya pili utakaotekelezwa Kwa kipindi Cha miaka mitano Hadi 2028 utagharimu zaidi ya shilingi Milioni 200 ambao utasaidia kutafikia masoko makubwa zaidi ya kikanda na kimataifa
Mkurugenzi wa Kampuni ya kitaifa ya kutoa huduma ya kuandaa mpango mkakati Kwa mashirika ya umma na yasiyo wa kiserikali Adolf Boyo amesema watahakikisha wanashirikiana kikamilifu na Bodi ya nafaka ili kuongeza tija katika sekta ya Kilimo
Pamoja ya mambo mengine katika utekelezaji wa mkakati wa awamu ya kwanza imebainika kuwa Wakulima wengi hawana taarifa zaidi kuhusu umuhimu wa kuhifadhi mazao yao kwenye maghala hivyo mpango huo wa pili utawawezesha Wakulima kuyafikia maghala hayo ili kuhifadhi nafaka zao