Alhamisi , 14th Jul , 2022

Naibu Waziri wa Kilimo  Anthony Mavunde ameitaka Taasisi ya Utafiti Kilimo (TARI) na wadau wengine wa kilimo kutoa elimu ya matumizi sahihi ya mbolea ili kumsaidia mkulima wa Tanzania kulima kwa tija

Naibu Waziri wa Kilimo  Anthony Mavunde

Naibu Waziri Mavunde ameyasema hayo leo Hombolo-Jijini Dooma wakati akitembelea mashamba ya mtama yanayofanyiwa majaribio kwa mbolea kutoka kiwanda cha ITRACOM FERTILIZERS kinachojengwa Nala,Dodoma.

“Mh Waziri Bashe alitoa maelekezo kwamba wataalamu wa TARI na TFRA mkae pamoja na kiwanda ili kufanya majaribio ya mbolea hii kutokana na ikolojia ya nchi yetu ili mbolea itakayozalishwa iweze kukidhi mahitaji ya udongo wa mbalimbali ya nchi.

Leo nimekuja hapa kushiriki zoezi hili la kutembelea mashamba ya mtama ya majaribio kujionea jinsi mbolea hii inavyofanya kazi katika zao la mtama.

Wadau wa kilimo mna wajibu wa kuielimisha jamii juu yaa matumizi sahihi ya mbolea kwa lengo la kuinua kilimo na kuongeza uzalishaji wa mazao yetu.

Katika kuchochea matumizi ya mbolea,serikali itatenga Tsh 150bn kama ruzuku ili kumpunguzia mzigo wa bei mkulima,sambamba na kuchochea ujenzi na uanzishwaji wa viwanda vya mbolea nchini”_Alisema Mavunde