Jumatano , 29th Sep , 2021

Taifa la China ni miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kwenye upande wa Teknolojia na hivi karibuni wameweka rekodi mpya baada ya kufanikiwa kutengeneza ‘Plasma’ ya nyuzi joto Milioni 120 kwa sekunde 101 na joto la Milioni 160 Celcius kwa sekunde 20.

Picha ya mradi wa International Thermonuclear Experimental Reactor (ITER)

Kituo hicho cha utafiti ni sehemu ya mradi mkubwa wa dunia “International Thermonuclear Experimental Reactor” (ITER), ambapo nchi nyingi zinashiriki kufanya majaribio ya kutengeneza nishati salama inayotokana na ‘nuclear fusion’ na itaanza kufanya kazi mwaka 2035 kwenye nchi kama 35.